Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, kutokea Tehran, Sheikh Naeem Qasim alisema katika hotuba yake katika mnasaba wa kumbukumbu ya Makamanda waliouawa Shahidi: Haji Imad Mughniyeh alikuwa shakhsia wa usalama na kijeshi na mvumbuzi, na aliongoza Mujahidina (wana mapambano ya Jihadi) kwa msingi wa imani.
Akaongeza: Jihadi lazima ifanywe ili kupiga vita batili na kuishinda. Hatutakata tamaa na wala hatutashindwa na wala hatutakubali kutawaliwa na batili.
Sheikh Naim Qassem aliendelea kusema: Rais wa Marekani Donald Trump anataka kufanya mauaji ya kimbari ya kisiasa kwa ushirikiano wa Netanyahu (Waziri Mkuu wa utawala haram unaoikalia kwa mabavu Palestina) ambaye alitaka kufanya mauaji ya kimbari ya Binadamu katika Ukanda wa Gaza lakini akashindwa na kufeli. Misimamo ya Trump kuhusu suala la Palestina ni hatari sana. Anataka kuiangamiza kabisa Palestina na Taifa lake.
Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon aliendelea: Upinzani (Muqawamah) ulifanya maendeleo makubwa sana tangu kuuliwa kigaidi kwa Sheikh Raghib Harb hadi kuuawa kwa Shahidi Sayyid Abbas Mousawi. Makamanda wa Mashahidi wanatembea tu katika njia ya Uislamu safi wa Muhammad (s.a.w.w). Njia yao ni njia ya upinzani (Muqawamah) wa Kiislamu. Jihad dhidi ya Israel ilikuwa ndio kipaumbele cha Makamanda wa Mashahidi.
Aliendelea kusema: Sifa ya makamanda waliouawa kishahidi ni hizi kwamba wanakusanya na kuchanganya Nyanja za kiroho na kidini sambamba na nyanja ya kijeshi.
Misimamo ya Donald Trump kuhusu suala la Palestina ni hatari sana
Kwa mujibu wa Al-Manar, Sheikh Naim Qassem, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon katika hotuba yake kwa mnasaba wa kuwakumbuka Makamanda waliouawa Shahidi ameashiria mpango wa Rais wa Marekani dhidi ya wananchi madhulumu wa Ghaza na kusisitiza kuwa, misimamo ya Donald Trump kuhusu kadhia ya Palestina ni hatari sana na anakusudia kuangamiza kadhia ya kisiasa ya Wapalestina.
Ameongeza zaidi: Mipango ya Trump (kuhusu Palestina) ni ndoto na njozi na haiwezi kutekelezwa.
Your Comment